Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni. Picha zote na OMR
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla.
Miili hiyo imewasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere – Terminal one (Air Wing) leo jioni majira ya saa kumi.
Mbali na Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, ni pamoja na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete.
Mara baada ya kuwasili miili hiyo iliongozwa na msafara kuelekea hospitali ya rufaa ya Jeshi, Lugalo, kwa ajili ya kuhifadhiwa hadi siku ya Jumatatu Julai 22, 2013 itakapoagwa rasmi kwa heshima zote katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga Jijini Dar es Salaam, ambapo ni Makao Makuu ya Jeshi Mkabala na Ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia majira ya saa tatu asubuhi.
Waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika mapokezi na hatimaye siku ya kuaga miili hiyo ya mashujaa wetu waliopoteza maisha wakitetea amani duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jioni.
Makamu wa Rais, Viongozi wengine waliofika kupokea Miili hiyo, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na mkewe, Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
Askari wakishusha majeneza yenye miili ya askari wenzao waliofariki dunia huko Darfur.
Baadhi ya wananchi waliofika kupokea na kushuhudia mapokezi hayo ya miili ya mashujaa wetu.
Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege.
Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akishikiliwa na wenzake wakati akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege.
Askari wa Jeshi wakijipanga kupokea miili hiyo kwa heshima.
Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege.
Nape Nnauye na Ridhiwan Kikwete, wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria.
Msafara wa magari ya Jeshi yaliyobeba miili hiyo ukianza safari ya kuelekea Lugalo.