Asalaam Alaykum kaka Othman!
Ni matarajio yangu kuwa umzima na waendelea kulisukuma gurudumu la utoaji habari kama kawaida kupitia katika nyanja zako kiilivyo na bado hujawa "mzigo kwa taifa".
Wajuwa kaka Othman,mimi hujisikia raha sana ninapoingia katika blog yako na kuanza kusoma habari za huko nyumbani.Hujihisi nipo poa kabisaaa lakini yajitokeza siku hizi kuwa blog yako yanivunja moyo na baadhi ya nyakati hujenga mawazo ya kuwa hamna mpya hasa. Maana ninapofungua hukuta habari "uporo" ambapo nyengine hubakia kama kwa siku 3-4. Waswahili wansema kipya kinyemi lakini kikuukuu kama ni kilaji huwa uporo na kama ni nguo huwa mtumba. Kiujumla kwa yote mawili hadhi na haiba hupungua kwa mtumiaji.
Ninachokushauri kama hamna (yaani wewe na crews) wako lakutuwekea jipya basi mie naona bora mbadilishe jina la blog yenu na kuiita zanzibar weekly news. Tutajuwa wasomaji kuwa twasoma habari za juma zima lililopita au tulilonalo.
Wajuwa masikio na macho yetu hujawa na mshawasha zaidi kusoma au kuona habari moto mto (mpya) yaani breaking news na ndipo kunakofanya kila wakati kutembelea blog lako lakini vyenginevyo ham na utwashi wa kutembelea huondoka. Jee itakuwa ni fahari kwako lipi kati ya mawili hayo kwa mtembeleaji wako blog hii awenalo.
Mimi siamini kuwa zanzibar (Unguja na Pembae) kuwa kuna uhaba wa habari moto moto mbona "mawio" wao hawazikosi,jee wao wanzitoa wapi,kulikoni !. Jaribuni ku up-date mara kwa mara kama wafanyavyo wakina Issa Michuzi ambapo ukikawia tu mada yayoyoma huikuti na kitu kipya chawekwa.
Nadhani kwa hayo ingawa ni mengi na nadhani hayakukuchosha kuyasoma namalizia kwa kusema kuwa kaza kamba ili haiba ipatikane katika blog yako.
Shukran na Wasalaam.