Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kilo 231,049 za samaki zavuliwa Wete

$
0
0
Na Masanja Mabula,Pemba
KILO 231,049 za samaki zenye thamani ya shilingi 549, 419,000, wamevuliwa katika kipindi cha mwezi Januari mwaka huu wilaya ya Wete kisiwani Pemba.
Afisa Uvuvi wilaya hiyo, Vuai Othman Haji, amebainisha hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi  ofisini kwake Kipangani.
Alisema samaki aina ya jodari na nduaro ndio waliovuliwa kwa wingi.
Alisema katika kipindi hicho, jodari waliovuliwa walikuwa kilo  67,050  wakiwa na thamani ya shilingi 236,724,000 na nduaro kilo  56,214 wenye thamani ya 188,756,000.
Aidha alisema samaki aina ya kangaja, vibua na dagaa waliovuliwa walikuwa na kilo  45,268 wakiwa na thamani ya shilingi 39,672,800  huku pweza na ngisi walikuwa na kilo 4,320 sawa na thamani ya shilingi 15,444,000.
Hata hivyo, alisema mafanikio hayo yamekuja kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Idara ya uvuvi, kamati ya wavuvi na wavuvi wenyewe.
kwa upande mwengine, alisema vitendo vya uvuvi haramu wa kutumia zana zisizoruhusiwa vimepungua na kuwataka wavuvi kuendeleza uvuvi unaozingatia hifadhi ya mazingira ya bahari.

Mwenyekiti wa kamati za wavuvi wilaya hiyo,  Mohammed Kombo, alisisitiza haja kwa wavuvi kuendeleza ushirikiano na Idara hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>