Na Muona Mbali
Ndugu wabunge la Katiba.
Mimi naguswa sana na matamko ya kikatiba.
Maana yangu ni kuwa katiba ikeshatamka ndio imetamka na ikikosa kutamka ndio inakuwa tayari haikutamka.
Kutamka inakuwa ni kama sheria ya kikatiba na inawezekana kutumika Mahakamani. Na kutotamka yaweza kudadisiwa mahakamani jee hilo limo ndani ya katiba? Yafaa kuiangalia kwa undani sana.
Nitagusia suala la kuchangia muungano chini ya serikali tatu.
Ikumbukwe kuwa idadi ya watu visiwani ni ndogo ukilinganisha na idadi ya watu Tanzania bara. Sasa inapokuja suala la michango ya muungano, basi bora katiba iainishe kima (yaani ratio) ngapi kwa ngapi.
Ninavyoona haiwezekani ikawa nusu kwa nusu. Hapo haki haitakuwepo.Na hiyo itakuwa ni mzigo mkubwa kwa Zanzibar. Na badala ya furaha ya kuwa na serikali 3 itakuwa ni madhila yaliyopindukia mipaka.
Sijui fedha za muungano zitakavyopatikana. How will it be generated, lakini kuna mifano ya matumizi tukiwacha matumizi ya kawaida.
Mfano kama Wizara ya Ulinzi inataka kununua jet fighters 10 nadhani si busara ununuzi huo na katika mchango wake utoke nusu zanzibar na nusu Bara na ndio hivyo hivyo labda katika ununuzi wa manuwari za kivita au makombora ya kileo. Ninachomaanisha hapa bado turudi katika katiba kama ni dira yetu jee mchango wa Zanzibar uwe ngapi na Bara uwe ngapi sio tusije kukorofishana baadae.
Pia hapo hapo katika share mfano wa Ofisi za Ubalozi nchi za nje kuwe na haki, maana leo kuna dosari kubwa. Mfano Ofisi za ubalozi nchi za nje kuna nchi very sensitive ambazo hizo kama ni kuzi-grade tunakuta ni zone A au band A. Mfano Uingereza, Marekani, Canada, Ufaransa na Ujerumani.
Leo utakuta kwa nchi hizi mabalozi wetu huko wote ni wazaliwa wa Tanganyika na ukichunguza Mzanzibari yupo wapi katika hizo hakuna,hapo hakuna haki, hilo ni kero la haki na ndio hivyo hivyo katika nchi band B.
Kuwe na mgawanyo mzuri tangu kwa mabalozi hadi watumishi wa balozi zetu. Na hii katiba itaje haki za mgawano tangu mwanzo (on the first place),la si hivyo haki haitakuwepo.
Nawazindua wabunge wateule wasisinzie wakienda huko na wawe imara.