Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe. Said Miraj. akihutubia katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya mpira Chukwani, akimtangaza Mgombea wake na kutowa Sera za Chama chake endapo itafanikiwa kikitowa kiti hicho cha Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, unaotarajiwa kufanyika kesho jumapili.
Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki wakifuatilia mkutano wa Chama cha ADC wakimwaga sera zake katika viwanja vya Chukwani.
Viongozi wakuu wa chama cha ADC wakiwa katika viwanja vya Chukwani wakihitimisha Kampeni yao ya kugombea kiti cha Uwakilishi katika Jimbo la Kiembesamaki, katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika kesho jumapili kumchagua Mwakilishi wao mpya baada ya Mwakilishi alieondolewa na Chama chake Mhe. Mansoor Yussuf Himid.