Kwa mujibu wa Ndugu wa Karibu wa Mhe. Haroun Ali Suleiman, wamekanusha taarifa zilizosambazwa kwa Wananchi wa Zanzibar kwa amefaridi dunia,Habari hizo sio kwele kwa na Jamaa na Ndugu wa Mhe Haroun wamekanusha habari hiyo kuwa ni uzushi, uliovumishwa na Watu wasiojulikana
Mmoja wa wana Familia amesama Ndugu yao Mwalim Haroun anaendelea vizuri na matibabu na hali yake inaendelea vizuri na kuzidi kuimarika .Mwalim Haroun amepelekwa Nchi Afrika Kusini kupata matibabu ya maradhi ya moyo. Na kwa sasa hali yake iko nzuri akiendelea na Matibabu yake katika hospitali Nchini Afrika Kusini.
Uvumi huu ulizagaa leo katika majira ya mchana kupitia njia ya SMS na kusambazwa kwa watu mbalimbali katika visiwa vya Zanzibar na vitongoji vyake na watu wengi wameshtushwa na taarifa hiyo isio kuwa na ukweli ndani yake
Wamesema Ndugu yao yuko Salama na anaendelea na matibabu yake. nchini Afrika Kusini.