Wananchi mbali mbali wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali na kumfariji Bi. Mkasi Jihadi wa Kijini Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wananchi wa Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali na kumfariji mzee Muombwa Rashid wa Kajengwa Makunduchi, wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja. (picha na Salmin Said, OMKR).

Na Hassan Hamad OMKR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, leo amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika ziara hiyo Maalim Seif amewaombea wagonjwa hao ambao ni watu wazima wapone haraka, pamoja na kuwataka wafiwa kuwa na subra katika kipindi hiki cha misiba inayowakabili.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wagonjwa hao wamemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuandaa ziara hiyo ya kuwafariji, ambayo wamesema inathibitisha kuwepo na upendo na ukaribu baina ya viongozi na wananchi.
Jumla ya wagonjwa na wafiwa 14 wametembelewa katika maeneo mbali mbali ya Wilaya za Kusini na Kati Unguja, yakiwemo Kizimkazi Mkunguni, Kijini Makunduchi, Jambiani na Ndijani.
Maalim Seif anatarajiwa kuendelea na ziara hizo za kuwatembelea wagonjwa na wafiwa katika mikoa yote ya Unguja na Pemba ndani ya kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.