Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkj.Ali Mohamed Shein,akimkaribisha tende Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi,wakati wa futari aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba jana katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Chake chake
Baadhi ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika chakula cha futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu ya Chakechake Pemba jana.
Baadhi ya Wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika chakula cha futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu ya Chakechake Pemba jana
Baadhi ya akina mama wa Mkoa wa Kusini Pemba wakiwa katika chakula cha Futari katika Mwezi mtukufu wa Ramadhan,iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa Ikulu ndogo ya Chakechake Pemba jana
Mke wa rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,(katikati) akijumuika na Wanawake wa Mkoa wa Kusini Pemba katika futari aliyowaalika jana katika ukumbi wa Ikulu ndogo ya Chakechake (kulia) Mkuu wa wilaya ya Chake chake Mwanajuma Majid
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,Juma Kassim Tindwa,akitoa shukurani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wake baada ya chakula cha Futari alkiyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Chakechake Pemba jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) pamoja na Viongozi na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kusini Pemba,wakiitikia dua iliyoombwa na baada ya chakula cha futari aliyoiandaa katika viwanja vya Ikulu ndogo ya Chakechake jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiagana na Wananchi mbali mbali wa Mkoa wa Kusini Pemba jana baada ya Chakula cha Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu ya Chakechake Pemba. {Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]
Na Rajab Mkasaba, Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein jana ameungana na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika futari maalum aliyowaandalia huko Ikulu ndogo ya Chake.
Akitoa shukurani kwa niaba ya Mhe. Rais Alhaj Dk. Shein, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Juma Kasim Tindwa alitoa shukurani kwa wananchi wote waliokubali mwaliko na kuhudhuria katika futari hiyo waliyoandaliwa na Rais ambayo imeonesha upendo mkubwa kwao.
Katika maelezo yake, Mkuu wa Mkoa huyo aliwasihi Masheikh katika Mkoa huo kuendelea kuhubiri amani na utulivu kwani hiyo ndio ngao pekee ya kujiletea maendeleo endelevu na kuishi katika maisha ya upendo.
Nao wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba wakitoa shukurani zao ambazo kwa niaba zilitolewa na Sheikh Mohammed Khamis na kueleza furaha za wananchi hao kwa kufutari pamoja na kiongozi wao wa nchi.
Katika maelezo yake Sheikh Khamis alitoa pongezi kwa Alhaj Dk. Shein kwa juhudi zake za kuwa karibu na wananchi katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo zikiwemo za kidini.
Wananchi hao walieleza kuwa katika uongozi wa Rais Dk. Shein wameweza kuona uongozi wa uadilifu anaoufanya pamoja na kutumia busara kubwa na unyenyekevu katika kuongoza nchi.
“Tumeweza kuona uadilifu wako mkubwa katika kuongoza nchi ikiwa ni pamoja na kushiriki katika shughuli mbali mbali za kidini zikiwemo ufunguzi wa misikiti katika maeneo mbali mbali”,alisema Sheikh Mohammed Suleiman.
Pamoja na hayo, wananchi hao walimtakia uongozi mwema kiongozi huyo na kuiombea nchi iendelee kuwa na amani na utulivu na kuwasisitiza wananchi kuendelea kushirikiana pamoja.