Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Matokeo yasiwalevywe wanafunzi darasa la saba, kidato cha pili

$
0
0
Na.Salum Simba, MUM                                                                   

 NAWAPONGEZA wanafunzi wa darasa la saba na kidato cha pili waliofanya vizuri mitihani yao lakini sijawasahau wanafunzi waliofeli wasivunjike moyo kwani kufeli kimasomo si kufeli kimaisha.                                                                                          

Waliofeli  wanayo nafasi ya kujiendeleza kimasomo na hatimaye kufanya vizuri masomo yao.

Wanafunzi waliopasi katika mitihani yao iliyotangazwa  hivi karibuni na waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali kwenye mkutano na waandishi wa habari inaonesha wazi kiwango kimepanda.

Nafikiri wanafunzi wanapaswa kusahau matokeo walioyapata wafanye juhudi ya kutosha ili kupata matokeo mazuri huko wanakokwenda, kwani tumesahau matokeo ya mwaka jana ya kidato cha nne zaidi ya asilimia 57 ya wanafunzi Tanzania walipata daraja ziro na kuhesabiwa hata aliyepata pasi mbili yaani “D” amefaulu hali ya kuwa hawezi kwenda popote kwa cheti chake.

Hapa tunapata funzo tusichekelee kwa kufaulu lakini tutathimini mitihani mingine kwani waswahili husema safari moja huanzisha nyengine, kwa hali hiyo juhudi zahitajika kwa kukamilisha safari hiyo.


Wanafunzi wengi hutumia nafasi walizozipata kulewa sifa za kupongezwa kwa kupasi kwao vizuri na kusahau wajibu wao wa kusoma kwa bidii. Aidha wanasahau kuwa ‘elimu ni ufunguo wa maisha’, ‘elimu ni nuru’.

Wengine utawasikia wakijisemea shida yangu ilikuwa kuvaa “black and white” hata nikifeli mtihani wa kidato cha nne nishazivaa na mimi nimetangazwa kwenye Radio ama wengine wanasema mtihani wa kidato cha nne na cha sita ni ya Tanzania bara hata nikijitahidi vipi nitafelishwa tu.

Nafikiri matokeo mabaya ya kidato cha nne na cha sita  yalitokana na kutochukua bidii katika masomo. Mbali na kuwepo sababu nyengine kadhaa zinazochangiwa na mazingira ya  masomo  lakini ifahamike hivyo



Wanafunzi ya wamekuwa wakitamani maisha anasa kama vile kumiliki simu za kisasa, nguo nzuri na mengine mengi, pia baadhi ya wanafunzi wanajihusisha na masuala ya mapenzi mapema jambo linalowaingiza katika maisha hatarishi na yasiyo salama ya kupata ujauzito na kupoteza haki yao ya masomo.

Matumizi  mabaya ya mitandoa ya kijamii kama vile facebook, viber, twiter na what is up (wasap) imewapotezea muda wao mwingi  ambao ungewafaa katika kudurusu masomo yao.

Ifahamike kuwa zaidi ya wanafunzi 80,000 wa chuo kikuu huhitimu kila mwaka, je wewe mwenzangu na mimi uliyrridhika na matokeo ya kidato cha pili na darasa la saba itakuaje katika soko la ajira?

Nina wasiwasi nikiyakumbuka matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana, kama wanafunzi wa Zanzibar hawatokuwa makini kwa kujiandaa kiume ili kukabiliana na mtihani hiyo tutakuwa tukipasisha wanafunzi wengi darasa la saba na kidato cha pili lakini tutakuwa tunafeli wengi kidato cha nne na cha sita kwa kulewa na kuridhika kwa matokeo tuliyoyapata hapo awali.

Wanafunzi wanapaswa kubadilika kwa kuyavua majoho ya sifa walizopewa na kupongezwa mitaani kwa kufanya vizuri lakini waliowapongeza watawasubiri tena kwa matokeo mengine.

Walimu nao wanapaswa kufundisha kwa kadri wawezavyo na wahisi wanafunzi wanaowafundisha ni sawa na watoto wao au ndugu  badala ya kuwapa maneno ya kuvunja moyo.

Baadhi  ya walimu wamekosa uvumilivu, ubunifu busara na hekma katika ufundishaji hali ambayo inapelekea wanafunzi kufanya vibaya masomo yao kwasababu walimu wengi kushindwa kutumia taaluma za kisaikolojia walizozipata wakati wanajifunza fani ya ualimu.

Natambua wazi na wala hakuna kificho kuwa walimu ni mihimili bora kwa maisha yetu kwani hata mimi binafsi nisingeweza kupata taaluma hii kama kusingekuwa na juhudi za walimu kutumika kwa kunifundisha kwao misingi bora ya kisoma kwa bidii.

Ipo haja kwa kila mmoja kuchukua juhudi kuimarisha elimu ili  kuleta matokeo yaliyo bora kwa wanafunzi.

Email:salumsimba@gmail.com, Tel: 0774 37 38 85 au 0712 04 51 19.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>