Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wizara yakana Wabunge kulipwa 160m/-

$
0
0
Na Mwandishi wetu
WIZARA ya Fedha na Uchumi imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba waziri wa wizara hiyo ameidhinisha ongezeko la malipo ya pensheni ya Wabunge hadi kufikia shilingi milioni 160 baada ya kustaafu.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wizara hiyo,Ramadhan Mussa Khijjah, alisema taarifa hizo ni za upotoshaji zenye lengo la kuwachonganisha Wabunge na wananchi wao.
Taarifa hiyo imesema waziri hajawahi kuzungumza na mwandishi wa habari yeyote kuhusu suala la nyongeza ya pensheni ya Wabunge na maelezo kwamba alithibitisha taarifa za ongezeko hilo sio na kwamba suala hilo halipo serikalini wala bungeni.
Taarifa hiyo iliwataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>