Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Jaji alaani mahakimu kushambuliwa

$
0
0
Na Rose Chapewa, MBEYA
JAJI  Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya,  Noel Peter Chocha, amelaani matukio ya kushambuliwa mahakimu wawili katika maeneo ya Tukuyu na Ileje jijini Mbeya na kusababishiwa ulemavu wa kudumu.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini, Jaji huyo alionesha kusikisitishwa na vitendo hivyo na kwamba wanafanya uchunguzi wa kina kubaini wahusika wa matukio hayo.
Alisema anashangazwa kuwa vitendo hivyo walifanyiwa mahakimu wa kike pekee ambapo mmoja alitobolewa jicho hivyo amelazimika kuwekewa  jicho la bandia.
Jaji huyo alisema ikiwa uchunguzi utakamilika na kuonesha kuwa zipo njama za makusudi za kufanya vitendo hivyo, mahakama haitasita kuuambia uongozi husika ili kusitisha huduma za kimahakama katika maeneo ambayo matukio yalitokea.
 "Tukifanya uchunguzi na kubaini kulikuwana njama za makusudi za kupanga kuwadhuru na kuwaumiza mahakimu, hakika hatutasita kuchukua hatua pamoja na kusitisha huduma jambo ambalo litakuwa ni hasara kwa wakazi wa maeneo hayo,” alisema.

Naye Wakili wa Serikali, kanda ya Mbeya, Edwin Kakolaki, alisema mahakama imeweka mikakati ya kuhakikisha mashauri ya muda mrefu yanamalizika mapema na kunakuwepo ripoti za kesi zilizoisha katika  vipindi mbalimbali vya mwaka wa mahakama.
Aliwaomba wadau wa mahakama ikiwemo magereza, jeshi la polisi na vyombo vingine vya upelelezi kuhakikisha kesi za jinai zinapelelezwa vizuri na kwa haraka, nyaraka mbalimbali zinapitiwa kwa uhakika na mashahidi kuandaliwa vizuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, aliwataka mawakili wa kujitegemea kupunguza gharama za uendeshaji kesi kwa wananchi kwa kuwa wengi wao kipato chao ni cha chini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>