Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Wizara yawatuliza walimu

$
0
0
Na Masanja Mabula,Pemba,
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mwanaidi Saleh, amewataka walimu kuwa wastahamilivu wakati serikali inajiandaa kufanya marekebisho ya  mishahara  kwa kuzingatia mpango kazi.
Alisema mpango huo utawawezesha walimu walioajiriwa miaka ya 1970 wenye vyeti  kunufaika na mabadiliko hayo  hali ambayo itaondoa malalamiko ya muda mrefu ambayo  yamekuwa yakitolewa na kuhusiana na mpango huo.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na walimu wakuu wa skuli za maandalizi , msingi na sekondari wa mkoa wa kaskazini Pembakwenye ukumbi wa Jamhuri Wete.
Aliema wakati wizara ikijiandaa kufanya marekebisho hayo, ni vyema walimu  wakuu mkoa huo kusimamia vizuri nidhamu kwa walimu ili kuwafanya waweze kutimiza majukumu ya kazi zao kwa ufanisi.
“Ni jukumu lenu walimu wakuu kuhakikisha walimu katika skuli zenu wanakuwa na nidhamu ya kazi ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango kazi kwa ajili ya wanafunzi kila siku,”alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utumishi wa wizara hiyo, Vuai Khamis Juma, aliwasisitiza walimu wakuu kuwasimamia vijana wanaoajiriwa ili waweze kujaza vyema mikataba yao.
Alisema wizara inatambua kuwepo na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya walimu juu ya tarehe zao za kuzaliwa.
Nao walimu wakuu wakichangia kwenye kikao hicho walihoji tafiti zilizotumika kubadilisha mitaala ya elimu kwa wafaunzi na kuongeza kwamba mwanafunzi wa darasa la kwanza kubebesha mzingo wa masomo nane ni vigumu kuyamudu.
Walisema  ni vyema wizara hiyo ikawapunguzia masomo wanafunzi hao ili waweze kuwa na uwelewa wa kutosha.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles