Na Muona Mbali
Nakumbuka Mh. Rais wa Muungano Jakaya Mrisho Kikwete alipotoa tangazo la mualiko kwa Taasisi gani zipeleke majina ya watu kuingia katika Bunge la katiba, aliyataja makundi 10 tu hayakuzidi.
Kuzuka kundi lisiloalikwa na likachaguliwa basi ni nje ya utaratibu alioutangaza awali Mheshimiwa Rais. Ima alikuwa aongezee kwa kulitangaza kundi hilo au kufuta kulitangaza au kufuta kuliteuwa.
Jana yalipotoka majina ya walioteuliwa, limejitokeza kundi la "mapendekezo binafsi", hili pia halikuwemo.Na kinachosikitisha zaidi kateuwa watu 118 na wote ni kutoka Bara. Jee wako wapi Wazanzibari?. Jee hapa haki imetendeka?
Mimi muona mbali naona pameteuliwa kiupendeleo ili kujaza nafasi tu kama ni hadaa.Hivi kama kundi hili la watu kujipendekeza binafsi kama lingelitangazwa jee wazanzibari wasingelijitokeza?
Mimi nahisi ima Raisi alifute kundi hili au aliweke lakini ajaze idadi alau nusu kutoka Zanzibar.