Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

MSANII NEMO KUPIGA SHOO LADY IN RED 2014

$
0
0
Na Andrew Chale
MKALI  wa R&B na Afro Pop,  ambaye aliwahi pia kushiriki shindando la BSS,  Nemo, anayetamba na wimbo wa ‘My Number One’ aliyomshirikisha Ommy Dimpoz anatarajia  kupafomu kwenye  shoo ya miaka 10 ya onyesho la mavazi lijulikanalo kama ‘Lady in red Super brand, 10th Anniversary’ linalotarajiwa kufanyika Februari 14, kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions inayoandaa onyesho hilo , Asia Idarous Khamsin, alisema tayari msanii huyo ameingizwa kwenye listi ya wasanii watakaotoa burudani kali nay a aina yake siku hiyo ya Februari 14.
Asia Idarous alisema msanii Nemo  anatarajia kuimba vibao vyake mbali mbali vikiwemo vya “Vumilia”, “Wife” na wimbo ulio kwenye chati ndani na nje ya Tanzania unaotamba kwa sasa wa  “My Number 0ne”.
“Hii ni ‘Surprise’ kwa wapendanao  katika onyesho letu la Miaka 10 ya jukwaa la Lady in red’ hivyo mbali na kushuhudia mavazi ya ubunifu yaliyobuniwa na wabunifu magwiji na wale wanaochipukia kwenye fani hii, pia watakonga nyoyo zao kwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa Msanii Nemo” alisema Asia Idarous.
Aidha, katika onyesho hilo, mbali na  Nemo,  pia kunatarajia kuwa na burudani kutoka mwanamuziki wa nyimbo za asili, Wanne Star na bendi ya Babloom Trio.
 Kwa upande wa wabunifu magwiji watakaopamba steji hiyo  siku hiyo ni pamoja na Mustapher Hasanal , Ally Remtulla, Lucky Creation, Martin Kadinda, Ghymkana Hilali,  Paka wear, Gabriel Molel, Fransiska Frankoo,  Shirima, Salim Ally, Ameed Abdul, Mgese Makory, Kiki Collection, Rose fashion, Diana Magesa, Rio Paul na wengine.
 Kwa upande wa wabunifu chipukizi: Faustin Simon, Water Edward, Brian Hango, Benedict Mnzava,Crissiwelly Uissoson,Willex Willibard, Jackson, Gumbala, Jabir Jumanne, Alabama King, Agusta Masaki, Nelson Tomas, Bebi Juliet Mtandu, Ummi fashion/Ummi Investiment Comapany, Asmahan Eva, Hassan Nasor, Juniper Mafuru, Ante Ngongi, Adam Hassan, Jaquline, Kijangwa na Waiz Shelukindo.
Katika onyesho hilo ambalo litafanyika siku hiyo ya Februari 14, ambayo pia itakuwa ni siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ , kiingilio kitakuwa sh 30,000 kwa viti vya kawaida huku viti maalum ikiwa sh 50,000. Tayari tiketi za onyesho hilo zimeanza kuuzwa ikiwemo vituo vya duka la Fabak fashion, lililopo mikocheni mkabala na kituo cha Mwalimu Nyerere huku kwenye hoteli ya Serena, zikipatikana mapokezi.
 Kwa mwaka huu onyesho hilo limedhaminiwa na adhamini mbalimbali wakiwemowadhamini wakuu ambao ni kinywaji cha Zanzi pamoja na kampuni ya nywele ya Darling.  Wengine ni CXC, Times fm, Clouds media, Vijimambo blog, michuzi media group, channel ten, Elite Computer, Eventlites, One touch-solution, Raysa Style, Paka Wear, Dj Bula, Magic fm, DTV, Jambo Leo, I View media, Vayle Spring, Voice of American na wengine wengi.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>