Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Zantel yazindua Kampeni mpya ya kuhamasisha usajili wa laini za simu

$
0
0

Dar es Salaam, Tanzania, 18-02-2014: Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imezindua zoezi la kuhamasisha wateja kusajili laini zao za Zantel kwa mujibu wa sheria ya serikali inayozitaka kampuni za simu kufanya usajili wa wateja wao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, kampeni hiyo inalenga kutambua wateja wote wanaohudumiwa na Zantel, lakini pia kusaidia kupunguza matumizi 

mabaya ya huduma za mawasiliano, na kuwapa wateja usalama katika shughuli kama simu benki, usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu na malipo kwa njia ya elektroniki kwa ajili ya huduma kama maji, umeme na kulipia huduma za luninga.

‘Lengo kubwa la kampeni ni kuhakikisha watumiaji na wateja wanao jiunga na Zantel wana tambulika na kupewa huduma bora na kampuni yetu’ alisema Pratap Ghose, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel.

Usajili wa laini za simu ni wa lazima kutokana na sheria ya mawasiliano ya 2010 ‘Electronics and Postal Communication Act’ (EPOCA), na chini ya sheria hii ni kosa la jinai kuuza au kusambaza laini ya simu ambazo hazijasajiliwa. Kutumia laini za simu zisizosajiliwa na kushindwa kurekodi mauzo ya laini za simu na kutoa taarifa za uongo wakati wakufanya usajili wa laini za simu.

Kulingana na kipengele 130 m (1) cha EPOCA 2010, mtu yeyote anaeuza au kwa njia yeyote anatoa simu za mkononi au laini za simu kwa mtu mwingine yeyote kwa njia sahihi ya sheria bila kurekodi taarifa za mtu huyo ana fanya kosa la jinai, na mtu huyo akitiwa hatiani ata takiwa kulipa faini ya shilingi milioni tatu au kwenda jela.

Sheria hiyo pia inamtaka mteja au promota wa laini za simu ambae kwakujua anatumia au ana sababisha matumizi ya laini za simu zisizo sajiliwa ana fanya kosa la jinai na akitiwa hatiani ata takiwa kulipa faini isiozidi 500,000/- au kifungo cha jela kisicho zidi miezi mitatu.

‘Tunawaomba watumiaji wote ambao hawaja sajili laini zao za sim kufanya hivyo haraka na kwa wale wanaotaka kujua hali yao ya usajili wapige *106#, ili waweze kuendelea kufurahia huduma mbalimbali za Zantel’’ alisisitiza Pratap.

Kwa kuongezea Pratap alisema ‘Sasa Zantel imerahisisha kwa wateja wake kusajili kwa kuongeza vituo vya mawakala wa Ezypesa, na maduka na ofisi za Zantel nchi nzima’
Ili waweze kusajili laini za simu, watumiaji wanatakiwa kutoa majina yao kamili, namba ya kitambulisho (cha aina yoyote), anuani ya posta, jinsia, tarehe ya kuzaliwa na namba za simu.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>