Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kutoka Bungeni Dodoma Wagombea wa Nafasi ya Muda ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Tanzania.wapigiwa Kura jioni hii.

$
0
0
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Yahya Hamad Khamis, akitowa maelezo ya kumpata Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ili kuwezesha kupata Kanuni za kuendesha Bunge hilo wakati wa Kikaochake baada ya kufanyika Uchanguzi wa Mwenyekiti wa Bunge hilo na Makamo Mwenyekiti wake. Na kutaja Wajumbe waliojitikeza kuomba Nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Muda waliojitokeza ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mbunge wa Jimbo la Donge Mhe. Sadifa Juma Khamis, Mhe, Magdelina Rubangira, na Profesa Costa Mahalu. ndio walioomba nafasi hiyo ya muda.  
Wajumbe wa Bunge Maalumla Katiba wakifuatilia maelezo yakiwasilishwa na Makatibu wa Bunge na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ya Tanzania wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia na wakipiga kura ya kumchagua Mwenyekiti wa Muda wa Kikao hicho kumpata Mwenyekiti wa Muda wa kuendesha Kikao cha Bunge la Katiba kuweka Kanuni za kuliendesha Bunge hilo.
Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Pandu Ameir Kificho akijieleza mbele ya Wajumbe wa Bunge la Maalum la Katiba, kuomba kura zao ili kumuwezesha kuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo katika hatua ya kuweka kanuni za Kikao hicho.wakati wa kumpata Mwenyekiti na Makamo wake kuliedesha Bunge hilo Maalum la Katiba Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Donge Zanzibar Mhe Sadifa Juma Khamis, akijieleza katika ukumbi huo kuomba kuchagulia na Wajumbe wa Bunge la Katiba, lakini baadae amejitoa katika kugombania Nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Muda.na kubaki Wagombea watatu.
Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Muda Mhe. Magdelina Rubangira, kutoka Asasi za Kiraia, akijieleza kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania, kuomba ridhaa zao kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania.  
Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Muda Mhe. Costa Mahalu.akijieleza kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania, kuomba ridhaa zao kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania.  

Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Thomas akitowa maelezoya jinsi ya ugawaji wa kura na upigaji kura wakati wa zoezi la kupiga kura ya kumchagua Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba Dodoma akiwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Yahya Khamis Hamad. wakisimamia zoezi hilo.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>