Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Tahadhari ya mvua kubwa

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Simu: 255 22 2460735/2460706

FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056

Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM

Tovuti: www.meteo.go.tz

Unapojibu tafadhali nakili:

Kumb. Na.: TMA/1622 18 Februari, 2014


Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa. Taarifa Na. 201402-03
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 8:30 Mchana
Daraja la Taarifa: Tahadhari
Kuanzia:
Tarehe
19 Februari, 2014
Mpaka:
Tarehe
21 Februari, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24) kwa siku
Kiwango cha uhakika: Wastani (60%)
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika Kanda ya kati (mikoa ya Singida na Dodoma), nyanda za juu kusini-magharibi (mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe) na maeneo ya kusini (Mikoa ya Ruvuma na Morogoro).
Maelezo: Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika rasi ya Msumbiji. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka misitu ya Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.
Angalizo: Idara zinazohusika na hali ya tahadhari pamoja na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>