Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Uteuzi wa Meneja Msaidizi EMS Dar ulifanyika kwa uwazi

$
0
0
 
Na Mwandishi wetu
 
SHIRIKA la Posta Tanzania limesema mchakato wa kuteua Meneja Msaidizi wa EMS wa Mkoa wa Dar es Salaam, ulifanyika kwa uwazi ambapo usaili ulifuata taratibu na kanuni zote ikiwa ni pamoja na kutangaza nafasi hiyo kwa wafanyakazi wa Shirika. 

Aidha zoezi la uchambuzi wa maombi lilizingatia sifa za waombaji ambapo msisitizo ulikuwa ni weledi, uadilifu na uzoefu katika kusimamia uendeshaji wa huduma na biashara ya  EMS courier & express. 

Taarifa ya Shirika hilo imesema wale ambao uchambuzi na upekuzi ulionyesha kuwa wanazo sifa zinazohitajika, waliitwa kwenye usaili. 

Taarifa hiyo imesema baada ya usaili,Conrada Makumbi, aliteuliwa kushika wadhifa wa  Meneja Msaidizi EMS mkoa wa Dar esSalaam.

Iliongozea Makumbi aliyetumikia Shirika la Posta na Simu na sasa Shirika la Posta kwa miaka 25, amepata mafunzo ya shughuli za Posta ndani na nje ya nchi na kabla ya hapo  alikuwa ni Ofisa Mwandamizi Mkuu kwa miaka 9.


Kuhusu mkataba na kampuni ya Technical  Mercantile, tarifa hiyo ilisema shirika liliingia mkataba na kmpuni hiyo kwa ajili ya kusimamia maegesho ya magari, kufunga, kupakia na kupakua mizigo katika Posta Kuu ya mkoa wa Dar es Salaam na kwamba mkataba ni halali na ulizingatia taratibu za kisheria na kisera.

Aidha iliongeza kwa sasa Shirika linafanya maandalizi ya kumpata mkandarasi atakeingia mkataba wa kutoa huduma husika kwa ubora unaokubalika. 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Shirika linaheshimu na kuthamini jukumu la vyombo vya habari katika kuhabarisha na kuelimisha jamii na mchango wake katika kuibua mambo mazuri na maovu miongoni mwa wana jamii.

Hata hivyo, limewaomba wana habari kuzingatia wajibu wao wa kuandika habari kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya uandishi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>