Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Hadithi ya leo (10)

$
0
0

 

Kutoka kwa Ummul Muuminiyna ‘Aaishah, Allaah amuwie radhi amesema:

( كَانَ يَعْتَكِفُ الْعَشْرَ الأَوَاخِرَ مِنْ رَمَضَانَ حَتَّى تَوَفَّاهُ اللَّهُ ، ثُمَّ اعْتَكَفَ أَزْوَاجُهُ مِنْ بَعْدِهِ )

ومسلم رواه البخاري

Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam alikuwa akifanya i’itikaaf katika kumi la mwisho la Ramadhaan hadi mauti yalipomfika. Kisha wake zake waliendelea kufanya i’itikaaf baada yake

Imepokewa na Bukhaari na Muslim

I’itikaaf ni mojawapo ya ibada muhimu ambapo muislamu hujitenga na dunia na kujifunga na msikiti kwa ajili ya kumuabudu Allaah Subhaanahu Wata’ala pekee.

Hukumu yake ni Sunna ila Sunna hii ni mojawapo katika Sunna ambazo zipo hatarini kutoweka endapo waislamu ambao ni mimi na wewe hatutakuwa tayari kuihuisha ibada hii muhimu ambayo Mtume wetu na ruwaza yetu alikuwa akiitekeleza kila Ramadhaan na wala hakuiacha mpaka wakati wake wa kuondoka duniani ulipowadia.

Kuna hadithi nyingi zinazozungumzia fadhila za I’itikaaf lakini Maulamaa wa hadithi wanasema nyingi ni dhaifu hivyo kabla ya kuitumia hadithi yoyote yenye fadhila za I’itikaaf hakikisha hukumu ya hadithi yenyewe kwanza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>