Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kaya 300 Kufanyiwa Utafiti wa Ukatili kwa Watoto na Kinamama.

$
0
0
Na Joseph Ngilisho,Arusha
KAYA 300 za watu wanaoishi na Ukimwi zilizopo Halmashauri tatu mkoani Arusha, zinatarajia kufanyiwa utafiti juu ya ukatili kwa watoto na kinamama waliopo ndani ya familia, ili kuangalia uwezekano wa  kupunguza ukatili huo.

Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Mratibu wa Ukimwi kutoka hospitali ya Selian, John Laizer, wakati akizungumza na wadau mbalimbali waliojumuika kutoa mawazo yao juu ya vitendo vya ukatili, vinavyofanywa  na baadhi ya wanajamii.

 Alisema wanawake na watoto wanaoishi ndani ya familia, baadhi yao wanapata mateso makubwa ya kupigwa,kudhalilishwa na kuvunjwa mikono, kutokana na baadhi ya kinababa kuwa na tabia ya kuwapiga.

Alisema vipigo hivyo vinawaathiri kisaikolojia watoto, hali inayosababisha kuwachukia baadhi ya wazazi wao, huku wengine kukimbilia mitaani, kutokana na kuchukizwa na tabia za unyanyasaji.

 Alisema utafiti huo unatarajia kufanyika muda wowote kuanzia sasa na utajulikana kwa jina la nyumba aminifu, utakaojumuisha halmashauri tatu za Arusha mjini, Arusha vijijini na Monduli na utalenga kaya  zilizoathirika na Virusi vya Ukimwi.


Alisema utafiti huo utafanyika kwa kushirikiana na Shirika la Savanna, Selian na kutumia viongozi wa mila na dini, ili waweze kutoa ushirikiano na kupata majibu sahihi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>