Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

TFDA yalipiga kufuli soko kuu Moshi

$
0
0
Na Kija Elias, Moshi.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA), imelifunga kwa soko kuu la Moshi , baada ya kubainika kutokidhi viwango vinavyotakiwa na hivyo kusababisha afya za watumiaji wa soko hilo kuwa hatarini kwa magonjwa ya mripuko.

Mamlaka hiyo iliagiza kufungwa kwa soko hilo kutokana na uchafu uliokithiri na kwamba maeneo ambayo yanatolewa huduma ya kuuzia nyama ni machafu mno.

"Mamlaka tumeamua kulifunga soko hili kwa sababu ya afya za watu, soko ni chafu, halina  miundombinu ya maji taka,  na mabucha ya nyama ni machafu sana hayakidhi viwango vya kutolea huduma,” alisema.

Kwa upande wao  wafanyabiashara wa soko hilo, wamekiri kuwepo uchafu ndani ya soko hilo, huku wakiitupia lawama ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri kwa kushindwa kuwapa taarifa na hivyo kuwashtukiza huku wakiwa tayari wamesha kopa mikopo mabenki,” walisema.


Wafanyabiashara hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe,wamedai agizo hilolimekuwa la kushutukizwa na kwamba litasababisha hasara kubwa.

 Aidha walisema kufungwa kwa soko hilo imekuwa adhaabu kwao kwani wanatengemea biashara hiyo kuendeshea familia, ikiwemo kuwasomesha watoto.

Akizungumzia suala hilo, Kaimu Mkurungenzi wa Manispaa ya Moshi, Dk. Christopher  Mtamakaya,  amekiri kuwepo taarifa za kufungwa soko hilo.

Alisema manispaa  hiyo imetenga  fedha  zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya ukarabati wa soko hilo, ambapo kwa sasa wako katika hatua za kumpata mkandarasi.

Alisema wafanyabiashara hao watahamishwa katika soko la Kiusa ambalo limefanyiwa ukarabati  na lina nafasi kubwa ili kupisha ukarabati.

Meya wa manispaa ya Moshi, Jafari Michael, ametofautiana na Mkurugenzi huyo kwa madai fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukarabati soko hiloni shilingi milioni 75 ambapo hadi  ukarabati kukamilika zinahitajika shilingi milioni 280.

Alisema ni vyema manispaa ikatafuta utaratibu mzuri wa kuwaondoa wafanyabiashara kuliko kutumia utaratibu ambao wameutumia wa kuwafungia kabisa wasifanye biashara.

Kwa upande wake diwani kata ya Kaloleni,  Michael Mwita, alisema barazala  madiwani, halijawahi kujadili suala hilo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>