Na Amina Omari,Tanga.
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais,Ummy Mwalimu, amesifu jitihada zinazochukuliwa na taasisi za kibenki nchini hasa katika kuisaidia jamii kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo afya na elimu.
Alitoa kauli hiyo wakati akipokea vitanda saba vyenye thamani ya shilingi milioni tano kutoka benki ya NMB kwa ajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito katika jiji la Tanga.
Makabidhiano hayo yalifanyika kituo cha afya Makorora jijini Tanga.
Alisema msaada huo umekuja wakati muafaka ambao utawaondolea adha waliokuwa wakipata akina mama wakati wa kijifungua.
Aidha aliwataka akima mama wajawazito kuwa na utaraibu wa kuhudhuria vituo vya afya wakati wa ujauzito ili kujua maendeleo yao badala ya kuendelea kukaa majumbani.
Awali Meneja wa NMB tawi la Madaraka mkoani Tanga,Juma Mpitimbi, alisema benki hiyo imetoa vitanda hivyo ili viweze kuhudumia vituo mbalimbali vya jiji hiulo nambayo ni sera yake ya kuunga mkono shughuli za kijamii hususani afya.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego, alisema msaada huo umekuwa faraja kubwa kwa mama wajawazito.