Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Tume za Mipango zatakiwa kushirikiana

$
0
0
Na Ameir Khalid
TUME za Mipango za Zanzibarna  Tanzania Bara zimeshauriwa kufanya kazi kwa pamoja katika kupendekeza masuala mbali mbali yanayohusu utekelezaji wa malengo ya melenia.

Wakizungumza katika mkutano wa siku moja uliowashirikisha watendaji wa tume hizo na viongozi wa taasisi zisizo za kiserikali, ambao uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar, walisema ushirikiano ndio utakaosaidia kutekeleza malengo ya millennia ifikapo 2015.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili ripoti ya Tanzaniayenye mwelekeo wa kuwa na ajenda moja baada ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Wajumbe hao walisema licha ya mafanikio yaliyofikiwa katika mipango mbali mbali ya maendeleo, bado upo umuhimu mkubwa wa tume hizo kushirikiana kwa karibu ili kuona malengo mengine yanafanikiwa.
Walisema licha kuwepo baadhi ya mambo yaliyofanikiwa ikiwemo elimu, afya na barabara, lakini tatizo kubwa ni jinsi ya kupata huduma bora kama vile madaktari wa kutosha, walimu wa sayansi na wananchi jinsi ya kuweza kutumia miundombuni ya barabara katika kujileta maendeleo.

Walisema asasi za kiraia na serikali ni vyema zikafanya kazi kwa pamoja katika kupanga mipango inayokusudiwa kufikishwa Umoja wa Mataifa wakati wa vikao vyake, kwa kuzingatia kuwa, Zanzibar bado baadhi ya watu hawajafunzwa kutumia miundombinu.

Mapema akiwasilisha mada katika mkutano huo Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Biashara, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, alisema bara la Afrika bado lipo nyuma katika kutekeleza malengo ya melinia.


Alisema tayari mikutano mingi imefanyika kuanzia mwaka 2000 katika kujadili maendeleo, ambapo mikutano yote hiyo imerahisisha kuleta ajenda ya maendeleo kwa nchi, ingawaje kuna tatizo la utekelezaji wa mipango hiyo.   

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles