Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Z’bar yaongoza kuripoti udhalilishaji

$
0
0
Na Fatuma Kitima, DSM
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimesema ripoti ya utafiti wa ukatili  wa udhalilishaji wa kijinsia inaonesha Zanzibarinaongoza kwa matukio ya ukatili wa kijinsi.

Utafiti huo umeonesha idadi ya wasichana  wanaoolewa wakiwa na umri mdogo wa kati ya  miaka 15 hadi 19 nchini ni asilimia 2.8.

Akizungumza na wanahabari Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Bodi ya TAMWA, Gladness Munuo, alisema mafaniko ya utafiti huo Zanzibar yametokana na wahusika kuwa wawazi katika  kutoa taarifa zinazowahusu tofauti na Tanzania Bara ambako kumekuwa na urasimu.

"Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuangalia  kiwango cha matukio ya ukatili wa kijinsia  katika wilaya 14 za Tanzania Bara na sita za Zanzibar,” alisema.

"Utafiti ulijikita katika maeneo ya ubakaji, ukeketaji, vipigo, kutelekezwa wanawake na  watoto, mauaji ya vikongwe, ndoa na mimba za  utotoni,"alisema.
Alibainisha kuwa utafiti huo ulifanywa na wanahabari kwa muda wa siku 10 na kwamba umethibitisha bila Tanzania bado ina kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia.

Alisema matukio yaliyobainika wakati  wa utafiti ni pamoja na ndoa za utotoni, kuozwa kabla hawajajitambua, wanawake kupigwa  na kutukanwa, wanaume kutekeleza familia, ndoa  za mitala, vipigo na mauaji

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>