Na Zainab Atupae, PEMBA
TIMU ya ‘Combine’ ya mkoa wa kaskazini Pemba, imeendelea kuwa ugea kwa timu kama hiyo ya mkoa wa kusini Pemba, baada ya jana tena kukubali kichapo cha magoli 4-2, kwenye mchezo maalumu wa kusaka wachezaji watakaounda timu ya taifa ya Tanzania itakayoshiriki michuano ya mataifa ya Afrika 2015.
Katika mchezo wa awali timu ya hiyo ya mkoa wa kaskazini Pemba, ilikubali kichapo cha magoli 3-2, ambapo na mchezo mwengine wa pili pia uliofanyika uwanja wa Gombani timu hiyo iliendelea kuwa mtija.
Magoli ya timu ya Combine ya kusini Pemba yaliwekwa wavuni na na mchezaji Omar Juma, mnamo dakika ya 61, huku goli mengine matatu ypte yaliwekwa wavuni na mshambuliaji Mussa Ali dakika za 69,81 na 84.
Magoli mawili ya kufutia machozi ya timu ya Combine ya kaskazini Pemba, yaliwekwa wavuni na Hassan Rashid dakika ya 44 na goli lapili lilingizwa na mchezaji Suleiman Saidi dakika ya 60.
Kumalizika kwa michezo hiyo miwili ya kusaka wachezaji wa watakaounda timu ya taifa ya Tanzania, ambayo mwakani itashiriki michuoni ya mataifa ya Afrika, kambi ya timu ya kusini Pemba imevunjwa rasmi.