Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

ZSTC Pemba yawataka Wakulima waliopewa mikopo kurejesha fedha

$
0
0
Na Zuwena Shaaban-Pemba. 27/02/2014.

SHIRIKA la Biashara la Taifa la ZSTC liliwapatia mkopo wakulima wapatao 93 wa zao la karafuu Kisiwani Pemba kwa msimu uliyomalizika wenye thamani ya zaidi ya shilling milioni 200 kwa ajili ya shughuli za uokoaji wa zao hilo.

Alisema shirika limeamua kwa maksudi kutoa mikopo hiyo kwa lengo la kuokowa zao hilo lakini inasikitishwa kuona mpaka sasa wako baadhi ya wakulima ambao wameshindwa kurejesha mikopo hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali Afisa Mdhamini Shirika la Biashara la Taifa ZSTC Pemba Nd,Abdullmalik Mohammed Bakar amewataka wakulima hao ambao wamepatiwa mkopo huo kurejesha fedha hizo kwa mujibu wa makubaliano yao.


Alisema kuwa tokea kumalizika kwa shughuli za uwokoaji wa zao hilo ambapo msimu uliomalizika , mpaka sasa ni wakulima wa chache tu ambao wameamua kurejesha mikopo hiyo kwa hiyari yao.

“Tulitoa mikopo kwa wakulima kwa ajili ya kutekeleza ahadi ya muheshimiwa Rais wa Zanzibar wakati alipowatembelea wakulima wa zao la karafuu Kisiwani Pemba na kutaka wakulima hao waweze kusaidiwa kama kilivyo kiliyo chao kwa shughuli za uokoaji” alisema Afisa Mdhamini huyo.


Alieleza nd,Abdullmalik kuwa “makubaliano ni kumalizika kwa msimu tu fedha hizo zirejeshwe kwa ajili ya kufanyiwa shughuli nyengine,ila mpaka kipindi hichi imekuwa ni vigumu kwa baadhi ya kurejesha fedha hiyo ambapo ni kinyume ccha makubaliano yetu.”.


Alisema kuwa ilifika kipindi kwa wakulima hao hao kumueleza Rais wazi wazi kuwa wanataka ngalau wakopeshwe fedha kwa ajili ya uokoaji kutokana na upandaji wa vifaa vya uokoaji na kukodi mashamba ya mikarafuu hivyo shirika iliyonaukoumuhimu wa kufanya hivyo kutokana kuwa wananchi wengi wanategemea zao la karafuu katika kujiinuwa kiuchumi.


Akifafanuwa mgawanyo wa mkopo huo kwa wilaya zote za Pemba Nd, Abdullmalik alieleza kuwa Wilaya ya Wete ni wakulima 56,Micheweni 17,Chake Chake 5 na Wilaya ya Mkoani ni wakulima 15.

Pia Nd,Abdullmalik alisisitiza kwa wakulima ambao mpaka sasa hawajarejesha fedha hizo kuwa ifikapo mwezi march mwaka huu, Shirika litachukuwa hatua kali dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Wakati huo huo Mdhamini aliwapongeza wananchi kwa kwa kujitokeza kwa wingi kwa kuliokoa zao hilo na kuliuza katika Shirika la ZSTC ambapo ameeleza kuwa shirika limefanikiwa kununuwa jumla ya tani 4890 za karafuu zenye thamani ya shilingi Bilioni 69 hadi mwezi wa Februari mwaka huu.




Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>