Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Maalim Seif awafariji walioathirika na maafa ya bomu Unguja Ukuu

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais Mh. Maalim Seif Shareif Hamad akupata maelezo kutoka kwa Simai Hussein Hassa (kulia) ambaye ni miongoni mwa majeruhi wa bomu lililowalipukia wavuvu wa kijiji cha Unguja Ukuu (Picha Salmin Saaid, OMKR).
 
NA Khamis Haji OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amewafariji na kuwapa mkono wa pole wananachi waliofikwa na maafa ya kuripukiwa na bomu katika kijiji cha Unguja Ukuu, Mkoa wa Kusini Unguja.
Akizungumza na baadhi ya wathirika wa bomu hilo pamoja na familia zao, Maalim Seif aliwataka wawe na subira kufuatia tukio hilo, kwa vile hayo ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu, ambayo yanaweza kumkuta binaadamu yoyote.
Tukio la kuripuka kwa bomu hilo lililotokea mapema wiki hii limesababisha kifo cha mwananchi mmoja, Juma Abdalla Juma na wengine watatu kujeruhiwa na hivi sasa wanaendeela na matibabu.
Makamu wa Kwanza wa Rais amesema jambo la muhimu ni kuwaombea majeruhi hao wapone haraka ili waweze kuungana na familia zao na jamii katika shughuli za kila siku za kimaisha.

Aidha, Maalim Seif amewahimiza wananchi wote wa eneo la Unguja Ukuu kuchukua tahadhari pale wanapoona vitu vigeni na wasivichezee, kwa sababu eneo hilo mara kadhaa hutumika kwa shughuli za mazoezi ya kijeshi.
Naye, Simai Hussein Hassan ambaye ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupata matibabu hospitalini kufuatia mkasa huo, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa ipo haja wananchi wa Unguja Ukuu wakapewa taaluma zaidi, ili waweze kujilinda na majanga kama hayo.
Wengine waliojeruhiwa ni, Shaaban Khamis Abdalla na Pandu Haji Pandu ambao bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mnazimmoja.
Marehemu Juma Abdalla alifariki Jumanne iliyopita wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazimmoja mjini Unguja.
Marehemu pamoja na wengine waliojeruhiwa ni wavuvi na walijeruhiwa na biomu hilo wakati alipokuwa kwa fundi kwa ajili ya kuyeyusha chuma walichokiokota baharini kwa ajili ya kufanya nanga kwa ajili ya mashua yao, bila ya kujua kwamba chuma hicho kilikuwa ni bomu.

 Eneo la Unguja Ukuu lililopo katika Mkoa wa Kuisni Unguja ni maarufu kwa ajili ya shughuli za mazoezi ya kijeshi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>