Baadhi ya Matrekta yalitolewa na KAMPUNI YA SUMA JKT yalipokabidhiwa kwa Wizara ya Kilimo na Maliasili
Kanal Mohammed Abdallah Rex akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Kilimo na Maliasili, Nd. Juma Ali Juma
Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Kilimo na Maliasili, Nd. Juma Ali Juma akijaribu moja ya Matrekata yaliyoptolewa na Kampuni ya Suma JKT

Katika kukamilisha ahadi za Mh.Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kufanikisha azma ya mapinduzi ya kilimo Wizara ya Kilimo na Maliasili imeleta nchini Matreka 20 kwa malengo ya kuinua uzalishaji wa kilimo nchini.
Akikabidhi matrekta hayo kwa niaba ya kampuni ya SUMA JKT, Kanal Mohammed Abdallah Rex, aliitaka wizara ya kilimo kuyatunza na kuyafanyia matengenezo (Services) kila wakati unapofika.
Akipokea matreka 20 kutoa katika KAMPUNI YA SUMA JKT kwa niaba ya wizara ya Kilimo na Maliasili, Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Kilimo na Maliasili, Nd. Juma Ali Juma, aliishukuru Kampuni ya Suma JKT kwa kukamilisha ahadi yake kwa vitendo na kusema matrekta hayo yatasaidia kuinuw kilimo cha mpunga kwa visiwa vyetu vya Unguja na Pemba kuanzia msimu huu wa mwaka 2014.
Gharama ya matrekta ni milioni mia nane na arubaini
Makabidhiano yamefanyika Karakana ya matrekta Mbweni.