Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Oman yaadhimisha siku ya mageuzi leo. Yajivunia maendeleo makubwa chini ya Sultan Qaboos

$
0
0
MUSCAT, Oman
TAIFA la Oman leo linasherehekea siku ya mageuzi , inayoadhimishwa kila ifikapo Julai 23.

Katika kuadhimisha siku hiyo, kiongozi mkuu wa taifa hilo Sultan Qaboos Bin Saeed, ametoa msamaha kwa wafungwa 215 waliokuwa wamefungwa kwa makosa mbalimbali wakiwemo raia 139 wa nchi hiyo.

Waziri wa Kazi Sheikh Abdullah bin Nasser Al Bakri, ametangaza kuwa leo ni siku ya mapumziko kwa wafanyakazi wote wa serikali pamoja na sekta binafsi.

Oman inaadhimisha siku hiyo kujipongeza kwa mabadiliko makubwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliyopatikana tangu Sultan Qaboos aanze kuiongoza nchi hiyo Novemba 18, 1970.

Chini ya Sultan Qaboos, Oman imeshuhudia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo sambamba na kuinua hali za wananchi wa nchi hiyo.

Maendeleo hayo ni katika sekta za afya, viwanda, kilimo, elimu, biashara na nyenginezo, pamoja na kuimarisha usalama na hifadhi ya nchi na wananchi wake.

Aidha mabadiliko hayo yamezingatia kuwajengea mazingira mazuri wananchi kwa kutambua kuwa wao ndio rasilimali muhimu katika ujenzi wa taifa lenye neema na ustawi.

Katika hotuba zake mbalimbali, Sultan Qaboos amekuwa akisisitiza kuwa, “maendeleo sio lengo pekee, bali yana maana ya kumjenga binadamu ambaye ndiye chanzo cha ufanisi”.

Katika kuimarisha uhusiano wa kimataifa, Oman pia imefungua balozi katika zaidi ya nchi 150 na ni mwanachama wa zaidi ya jumuiya 100 za kimataifa duniani kote. (Oman Observer).






Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>