MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi. TUNAOMBA SANA MSAADA WENU MTOTO ATIBIWE KWANI ANATESEKA SANA MTOTO HUYU |
Baba wa mtoto huyo Joseph Njavike amesema wakati wa tukio yeye alikuwa hayupo nyumbani |
Mama mzazi wa Adorotea Milika Kibelege. |
Hatimaye Wazazi wa mtoto Adorotea Njavike mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne wamewasili Jijini Mbeya kutoka Mkoani Njombe baada ya kutafutwa kwa muda mrefu kutolea maelezo ya ajali ya mtoto aliyeungua moto miezi saba iliyopita.
Ajali hiyo imepelekea ulemavu mkubwa kwa mtoto huyo ambapo ngozi ya kidevu imeungana na kifua na kumsababishia ulemavu unaomfanya kushindwa kula vizuri na macho kushindwa kufumba.
Baba wa mtoto huyo Joseph Njavike amesema wakati wa tukio yeye alikuwa hayupo nyumbani kwani mtoto alibaki na mama yake mzazi aitwaye Milika Kibelege.
Milika amesema kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa mbili usiku alipokuwa anapika na yeye kupigwa na kitu kichwani kisha mtoto kudondokea motoni nay eye kuzirai kabla ya mtoto kuokolewa na majirani baada ya kusikia kilio kikali kutoka kwa mtoto.
Milika amesema kuwa baada ya tukio mtoto alikuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kijiji cha Wanzali na kwamba yeye alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo hali iliyomlazimu Dada yake kumchukua mwanae hadi Mbeya ili aweze kupatiwa matibabu zaidi.
Kutokana na uduni wa maisha wameshindwa kufika Mbeya kumjulia hali mtoto wao hadi walipofuatwa na Dada yake Machi 8 mwaka huu kuwa wanahitajika Mbeya ili kibali kitolewe mtoto asafirishwe kwenda Hospitali ya Mhimbili kwa matibabu zaidi.
Mama Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye alitoweka na mtoto huyo amesema anaomba radhi kwa kuondoka bila kuaga na mtoto huyo kwani alichanganyikiwa alipoambiwa mtoto itabidi asafirishwe kwenda India na matibabu yake yatachukua miezi sita hivyo akaona ni bora awafuate wazazi wa mtoto huko njombe wakajadiliane
Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya Thobias Mwalyego baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari alilazimika kwenda hadi mtaa wa Maendeleo Iyunga ili kupata maelezo ya kina kutokana na ofisi yake kutokuwa na taarifa zozote juu ya mtoto huyo.
Mwalyego amesema kuwa kuanzia sasa ataendelea kufuatilia maendeleo ya mtoto huyo kuhakikisha anapatiwa huduma zinzostahili ukiwemo msamaha wa matibabu kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kwa upande wa wazazi wamewashukuru wasamaria wema waliojitokeza kuchangia matibabu ya mtoto wao na madaktari wanaofanya juhudi za kuhakikisha mtoto huyo anapatiwa upasuaji wa haraka.
Aidha amekubali kuandamana na mwanae katika matibabu endapo ataruhusiwa kwenda kokote na Afisa Ustawi wa Jamii alishauri pia Mama mkubwa kuongozana na Familia hiyo kutokana na udhaifu wa mama Adorotea
Na Mbeya yetu