Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. John Samuel Sita akitoa neno la shukrani mara baada ya Tafrija fupi ya kupongezwa kwake yeye na Makamu wake Mh. Samia Suluhu hapo Chinese Restaurant Mjini Dodoma.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza katika Tafrija fupi ya kupongezwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mh. Moh’d Aboud Moh’d akizungumza wakati wa tafrija hiyo ya kuwapongeza Mwenyekiti na Makamu wake kwa kuchaguliwa kuliongoza Bunge Maalum la Katiba Tanzania ,tafrija hiyo imefanyika katika hoteli ya ya Dodoma hoteli Mgahawa wa Kichina.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Tanzania ambae pia ni Waziri wa Nchi anayeshughulikia Muungano Mh.Samia Suluhu Hassan Kushoto akiwa pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi katika Tafrija ndogo ya kuwapongeza Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo mara baada ya kuchanguliwa kuliongoza Bunge hilo linaloendelea kukutana Mjini Dodoma.
Washiriki wa Tafija fupi ya Kupongezwa kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh. John Samule Sita na Makamu wake Mh. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika Mkahawa wa China uliomo ndani ya Dodoma Hoteli.(Picha na Hassan Issa -OMPR)