Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHITIMISHA SHEREHE ZA MIAKA 10 YA SIKU YA PAI TANZANIA.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Maandamano ya Wanafunzi na Walimu wa Shule za Sekondari, Msingi na Vyuo Vikuu, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Siku ya Pai Tanzania, iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Maandamano ya Wanafunzi na Walimu wa Shule za Sekondari, Msingi na Vyuo Vikuu, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Siku ya Pai Tanzania, iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Julian Ilunga, wa Shule ya Sekondari Kitangili Mwanza,  aliyeibuka mshindi wa kwanza katika shindano la ‘Junior Mathematics Contest 2013’ wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya vitabu wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Pai Tanzania, leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na baadhi ya wanafunzi , wakati akiondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, baada ya kuhitimisha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania.

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana wakitoa burudani ya kwaya wakati wa sherehe hizo Mnazi Mmoja leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanafunzi waliofanya vizuri katika shindano la ‘Senior & Junior  Mathematics Contest 2013’, baada ya kuwakabidhi zawadi zao, wkati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Pai Tanzania. Picha na OMR


Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>