Mkutano wa 57 wa Kamisheni ya Umoja Wa Mataifa inayosimamia Dawa za Kulevya umeanza jana tarehe 13 March, 2014 katika Makao Makuu ya Kamisheni hiyo Vienna International Conference Center nchini Austria. Mkutano utajadili mikakati ya kupambana na uzalishaji na usafirishaji wa dawa za kulevya duniani.
Zanzibar imewakilishwa katika mkutano huo na Waziri Wa Nchi OMKR Mhe. Fatma A Ferej, Katibu Mkuu OMKR Dr. Omar Shajak na Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Uratibu na Udhibiti Wa Dawa za Kulevya Zanzibar ACP Kheriyangu M Khamis