Na Khamis Haji OMKR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesifu mwamko wa wanawake hapa Zanzibar katika kujiendeleza kielimu hali inayofanya idadi ya wanawake wanaohitimu katika vyuo mbali mbali kuzidi kuwa kubwa, ikilingansihwa na siku za nyuma.
Maalim Seif amesema hayo wakati akihutubia katika mahafali ya sita ya Chuo cha Utawala wa Umma yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho, kilichopo Tunguu, mkoa wa Kusini Unguja.
Maalim Seif amesema hali hiyo inadhihirisha ukweli kuwa wanawake wana uwezo mkubwa sawa au kuliko wanaume, na jamii ina wajibu wa kuhakikisha wanawake wanapewa fursa sawa ikiwemo za kielimu, zitakazo wawezesha kushika nafasi katika nyanja zote zikiwemo zile zinazohitaji utaalamu wa hali ya juu.
Hata hivyo, Makamu wa Kwanza wa Rais amesema ili kuweza kufikiwa azma ya kumkomboa mwanamke kikamilifu katika sekta ya elimu, mkazo mkubwa zaidi hivi sasa uwekwe katika kuwapa misingi ya elimu ya Sayansi na teknolojia, ili waweze kwenda sambamba na wakati uliopo.
“Tunataka tuwe na wataalamu wengi wanawake tena katika fani zote, zikiwemo sayansi na teknolojia, tuwe na marubani wengi wanawake, tuwe na wana jiolojia, tuwe na wahandisi. Lakini hili tutalifikia tukiweka mkazo mkubwa zaidi katika kuwasomesha masomo ya sayansi na teknolojia, alihimiza Maalim Seif.
Makamu wa Kwanza wa Rais amewahimiza wahitimu hao wakiwemo ambao tayari ni watumishi na wale ambao wanatarajiwa kuwa Watumishi wa Umma kuitumia ipasavyo taaluma waliyoipata chuoni hapo, ili kufanikisha Mpango wa wa mageuzi ya Utumishi wa Umma hapa Zanzibar.
Amesema mageuzi hayo yanalenga kuleta mabadiliko katika utoaji wa huduma kwa wananchi na kupiga vita tabia ya baadhi ya watumishi kufanya kazi kwa mazowea.
“Tukifanikisha magezu haya ndipo tutakapokwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya Ulimwengu, kasi ambayo inatokana na kukua kwa Sayansi na Teknolojia, lazima tubadilike na kubadilisha mfumo wetu wa utendaji kazi”, alisema Makamu wa Kwanza wa Rais.
Jumala ya wahitimu 1,463 walikabidhiwa vyeti na Stashahada katika fani za Utawala wa Umma, Usimamizi wa Rasilimali Watu, Uhadhili, Ununuzi na Ugavi, Mawasiliano na Habari (IT) na cheti cha Sheria.
Katika risala ya wahitimu hao iliyosomwa na Sharifa Suleiman, wametaja miongoni mwa changamoto kuu zinazokikabili chuo cha Utawala wa Umma kuwa ni uhaba wa walimu wa kudumu, usafiri, kukosekana uzio chuoni hapo hali inayosababisha mifugo kuvamia eneo la chuo na kukosekana maktaba inayokidhi mahitaji.
Khamis Haji, OMKR