Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Warioba kuwasilisha rasimu bungeni leo

$
0
0
Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, leo anatarajiwa kwenda bungeni kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba kwa wajumbe wa bunge hilo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa bunge, hilo Samuel Sitta, aliwambia wajumbe kuwa Jai Warioba atakaribishwa leo kuwasilisha rasimu hiyo kwa mara ya kwanza kwa bunge hilo.

Baada ya Jaji Warioba kuwasilisha rasimu, itakuwa zamu ya Rais Jakaya Kikwete kulihutubia bunge hilo Jumanne au Jumatano, kabla ya kazi ya kuchambua na kujadili kifungu kimoja baada ya chengine kuanza.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni za bunge hilo, Rais alipaswa kutangulia kulihutubia bunge hilokabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Mjumbe wa bunge hilo, ambae alishiriki kazi ya utungaji rasimu, Tundu Lissu, wiki iliyopita alimtikiza Mwenyekiti wa bunge, akisema amevunja kanuni kwa kuwatangazia wajumbe kuwa Jaji Warioba atakaribishwa Jumatatu wakati rasimu inataka Rais atangulie kwanza.

Akiomba mwongozo, Lissu alisema kanuni inamtaka Rais Jakaya Kikwete kulihutubia Bunge kwanza kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuwasilisha rasimu ya katiba bungeni.

“Mwenyekiti naomba mwongozo wako kuhusu tangazo lako kwamba Jaji Warioba atakuja kuwasilisha rasimu yake ndipo Rais aje kulihutubia Bunge, kanuni zetu zinamtaka Rais aje kwanza kulihutubia Bunge ndipo Jaji Warioba aje kuwasilisha rasimu yake.” 

“Tuliamua hivi kwa kuwa tuliona iwapo Jaji Warioba akitangulia kuwasilisha rasimu baada ya hapo ndipo Rais aje kulihutubia Bunge itaonekana kama Rais Kikwete amekuja kumjibu Mwenyekiti wa Tume,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa kanuni hizo, kazi ya kwanza inayotakiwa kufanywa na wajumbe inaanzia katika kamati zitakazoundwa na kuhoji Sitta ametumia kanuni ipi kuruhusu mjadala wa siku tatu.
Akijibu hoja hizo ya Lissu, Sitta alisema Rais hawezi kuja kulihutubia Bunge wakati hakuna ajenda yoyote iliyowasilishwa kwa wajumbe.
“Kwa uzoefu wangu katika bunge lazima kwanza tuwe na ajenda, Jaji Warioba atakuja kuwasilisha rasimu ili tuwe na ajenda mkononi ndipo Rais aje kulihutubia Bunge. Tumelijadili hili na wenzangu tumeona iwe hivyo ikiwezekana tutatengua kanuni kumruhusu Jaji Warioba kuwasilisha kwanza rasimu ya katiba kwa wajumbe,” alisema
Alisema kanuni zinamruhusu kutumia busara yake kuamua baadhi ya mambo kwa namna anavyoona inafaa hivyo ametumia madaraka yake kuamua hivyo ili wajumbe wawe na mjadala mpana kabla ya kwenda kwenye kamati.


“Katika kipindi hiki pia nitapata muda wa kuwajua wabunge na hivyo kuweza kuwapanga katika kamati mbalimbali, wajumbe zaidi ya 600 mliopo humu ni wengi lazima nipate muda wa kutafakari kabla ya kuunda kamati,” alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>