Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Madiwani CCM watishia kurejesha kadi

$
0
0
Na Joseph Ngilisho, ARUMERU
KATIKA hali isiyo ya kawaida Madiwani wa CCM katika halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani wa Arusha wametishia kujiuzulu pamoja na kukusanya kadi zote za chama kutoka kwa wananchi na kuongoza nao  kwenda kuchukua ardhi yao aliyokabidhiwa mwekezaji iwapo serikali haitatoa tamko.

Walitoa onyo hilo katika baraza la madiwani lililofanyika halmashauri hiyo ambapo, ajenda ya migogoro ya ardhi ilifanya baraza hilokujikuta likitoa tamko na vitisho vikubwa kwa watumishi wa halmashauri hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake, diwani wa kata ya Maroroni, Mwanaidi Kimu, alisema wamechoshwa kila siku kujadili ajenda za migogoro ya ardhi lakini hakuna utendaji wowote na badala yake wanabaki wakiwa na kumbukumbu ya vikao katika vichwa vyao hali ambayo kwa sasa imefika mwisho.

Akitolea mfano moja ya shamba lenye migogoro, alisema ni shamba la Madira lililopo maeneo ya Seela Singisi ambalo ni mali ya halmasahuri hiyo lakini kwa sasa kuna migogoro ambayo inasababishwa na baadhi ya viongozi wanaodai ni lao.
Akizungumza kwa niaba ya madiwani wanaume,Wilson Nyitti, alisema hali hiyo imesababisha kila wanapopita wakiwa wanazomewe na wananchi kwa kuwa wanafikiri wao wananufaika na migogoro hiyo.

Mwenyekiti wa halmasahuri hiyo ya Meru, Goodson Majola, alisema tamko hilo la kutaka kujiuzulu kwa madiwani wote 23 lipo sawa kwa kuwa migogoro yote ya ardhi inasababishwa na viongozi wasio waadilifu.

Akizungumzia shamba hilo la Madira alisema, Rais Kikwete tayari ameshatoa ardhi hiyo yenye hekari 360 lakini bado hawajaweza kulitumia kutokana na vitisho wanavyopewa

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>