Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

WIZARA YA BIASHARA ZANZIBAR YAPATA MSAADA KUTOKA WIZARA YA BIASHARA SMT

$
0
0

 
Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula kulia akimkabidhi Funguo ya Gari Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael,kushoto ni Elizabeth Lukaza Mchambuzi wa Shirika la UNDP Tanzania.Hafla imefanyika leo Wizara ya Biashara Zanzibar.
Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg Edward Sungula kulia akimkabidhi Vifaa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Ndg.Julian Raphael,hafla hiyoimefanyika katikaOfiza ya  Wizara ya Biashara Malindi  Zanzibar. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian Raphael kulia akitoa neno la Shukran baada ya Makabidhiano ya Gari na Vifaa kwa Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula.


 Na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar 25/03/2014

Wizara ya Biashara na Viwanda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi Gari na Vifaa vya Ofisini kwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Wizarani Malindi mjini Unguja.
Msaada huo uliofadhiliwa na Shirika la Biashara la Dunia WTO ulitolewa ili kuijengea uwezo Wizara ya Biashara ya Zanzibar katika kukabiliana na majukumu yake ya kila siku.

Akikabidhi Msaada huo Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Bara Edward Sungula kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael amesema Suala la Biashara ya Kimataifa ni la Muungano hivyo Serikali mbili lazima zishirikiane na kusaidiana katika kutekeleza majukumu yao.

Amesema Msaada huo ni utekelezaji wa Mradi wa “Capacity Building for Trade Development and Integration Project” ambao una lengo la kuzijengea uwezo Serikali katika kutekeleza misaada chini ya utaratibu wa “AID FOR TRADE”.

 Ameongeza kuwa msaada huo ni mwanzo wa kudumisha ushirikiano katika kutekeleza mradi huo na njia ya kuendeleza kudumisha Muungano uliopo baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian Raphael ameishukuru Wizara hiyo juu ya Msaada huo na kuongeza kuwa utachochea ufanisi katika majukumu yao.

Katika kutekeleza Mradi huo wa kukuza Sekta ya Biashara Tanzania Bara na Zanzibar Mradi umeanza kwa kununua Vifaa ambavyo ni pamoja na Gari mbili, Komputa, Projekta na Mashine ya Kuprintia.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>