Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Diwani wa Mzuri Awataka Wanafunzi kuachana na Mambo ya Anasa na Kushughulikia Masomo yao.

$
0
0
Diwani wa wadi ya Mzuri Kaja, Makunduchi, ndugu Zawadi Hamdu Vuai amewataka wanafunzi wa Skuli ya Kusini kuacha kujishughulisha na mambo ya anasa na badala yake wapanie kwenye masomo yao. Akizungumza kwenye sherehe za kuwapongeza wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha tatu na kidato cha tano, ndugu Zawadi amesema kuwa vitendo vya anasa kama vile kutumia muda mrefu kwenye televisheni kuangalia michezo ya sinema na mapenzi ni adui wa maendeleo ya elimu. Diwani huyo amewaasa wanafunzi kutumia muda wao  vizuri kwenye masomo yao. Katika picha kutoka kulia ndi sheha wa Tasani akifuatiwa na sheha wa Mzuri, mwalimu Mwita Masemo, msaidizi wa mwalimu mkuu, ndugu Mussa Nahodha; katibu wa jumuiya  ya Mzuri kaja, mwalimu Haji Nyimbo, mwandishi wa radio Mtegani na mwenyekiti wa kamati ya skuli ya Kusini ndugu Humudi Sago.
Wanafunzi wa Skuli ya Kusini wakimsikiliza kwa makini Diwani wa wadi ya Mzuri kaja, ndugu Zawadi Hamdu Vuai kari sherehe ya kuwazawadia sare wanafunzi 60 waliofaulu mitihani yao, kati yao wanafunzi 52 wamefaulu kuingia kidato cha tatu, wanafunzi 7 wataingia kidato cha tano na mwanafunzi mmoja ameingia mchepuo. Jumuiya ya Maendeleo ya Watu wa Mzuri kaja (Mzuri kaja Development Society) ndio iliyodhamini sare hizo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>