THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 Fax: 255-22-2113425 | PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Brussels, Ubelgiji leo asubuhi 2 Aprili,2014 kuhudhuria kikao cha siku mbili cha Wakuu wa Nchi wa nchi za Afrika na za Umoja wa Ulaya (EU-Africa Summit).
Kikao hiki cha siku 2 kitatoa nafasi kwa viongozi hawa kutathmini mafanikio ya uhusiano wao na kutafuta njia zingine mpya za kuboresha mahusiano hayo .
Kauli mbiu ya mkutano wa Mwaka huu inasisitiza katika kuwekeza kwa watu,Mafanikio na Amani (Investing in people, prosperity and peace) na baadaye kufanya mazungumzo na Rais wa Kamisheni wa Nchi za Ulaya (EU) Bw. Jose Manuel Barosso.
Akiwa Brussels Rais Kikwete anatarajia kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mheshimiwa Mark Rutte.
Rais Kikwete anatarajia kuondokaBrussels mara baada ya Mkutano kumalizika na kurejea Dar es Salaam.
Imetolewa na;
Kikao hiki cha siku 2 kitatoa nafasi kwa viongozi hawa kutathmini mafanikio ya uhusiano wao na kutafuta njia zingine mpya za kuboresha mahusiano hayo .
Kauli mbiu ya mkutano wa Mwaka huu inasisitiza katika kuwekeza kwa watu,Mafanikio na Amani (Investing in people, prosperity and peace) na baadaye kufanya mazungumzo na Rais wa Kamisheni wa Nchi za Ulaya (EU) Bw. Jose Manuel Barosso.
Akiwa Brussels Rais Kikwete anatarajia kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mheshimiwa Mark Rutte.
Rais Kikwete anatarajia kuondoka
Imetolewa na;
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Brussels , Ubeligiji.
2 Aprili, 2014
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
2 Aprili, 2014