Ujumbe wa Wafadhili kutoka Umoja wa Ulaya na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosaidia Wanawake wakipata maelezo ya kutoka kwa mmoja wa Mwanakikundi wa kijiji hicho.wakielezea jinsi ya upandaji wa mwani unaoendeshwa na Wanawake hao ikiwa ni moja ya miradi yao.
Mratibu wa Mradi wa kupambana na Ajira za Watoto Zanzibar Bi Mzuri Issa akisisitiza jambo kwa Wanakikundi wakati wa kukagua miradi mbalimbali inayofanywa na Kinamama hayo katika kijiji cha Uzini Wilaya ya Kati Unguja,
Wanawake wa kijiji cha Uzini ambao wanajishughulisha na biashara ndogondogo kupitia mradi wa kupambana na ajira za watoto wakiwa katika uandaaji wa biashara hiyo ya kufunga chaoro kwa ajili ya biashara kutunisha mfuko wao kupitia mradi huo.