Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mahakamani kwa kulawiti mtoto wa miaka 14

$
0
0
Na Shemsia Khamis, PEMBA
MAHAKAMA ya Mkoa Chakechake, chini ya Hakimu Khamis Ramadhan Abdalla, imempandisha kizimbani mshtakiwa Abuu Said Omar (15), mkaazi wa Wawi Chakechake, kujibu tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume (14), zilizomkabili mahakamani hapo.
Ilidaiwa mahakamani hapo, na Mwendeshamashtaka Ali Bilali Hassan kuwa, mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo, Machi 14 mwaka huu majira ya saa 7:00 mchana.
Mwendeshamashtaka alidai kuwa, mshtakiwa bila halali alimuingilia mtoto huyo kinyume na maumbile, katika mabonde ya Wawi mtegani, wilaya ya Chakechake.
Baada ya mshtakiwa huyo, kusomewa shitaka lake, alikana na kuiyomba mahakama impatie dhamana, kutokana na kuwa ni haki yake ya kisheria.
‘’Muheshimiwa Hakimu, naiyomba mahakama yako tukufu, inipatie dhamana kutokana na kuwa, ni mwanafunzi wa darasa la sita, hivyo nikienda rumande nitakosa kusoma’’, alidai mshtakiwa.
Kufuatia ombi hilo, Mwendesha mashtaka alidai hana pingamizi yoyote endapo mshtakiwa ataweza kutimiza masharti ya dhamana atakayopewa na mahakama.

Hakimu aliyataja masharti ya dhamana, kuwa ni pamoja na yeye binafsi kujithamini shilingi milioni 2,000,000 za maandishi na wadhamini wawili, kima kama hicho za maandishi.
‘’Mshtakiwa wathamini wako wawe na vitambulisho vya uzanzibar ukaazi na barua za sheha katika shehia wanazoishi ndipo tuweze kukupa dhamana’’, alisema Hakimu.
Baada ya mshtakiwa kuweza kutimiza masharti ya dhamana, bila ya pingamizi yoyote mahakamani hapo, ndipo Hakimu alipomuamuru mshtakiwa kwenda nje hadi siku hiyo.
Kwa mujibu wa sheria kufanya hivyo, ni kosa kinyume na kifungu cha sheria cha 150 (a), sheria namba 6 ya mwaka 2004, sheria ya Zanzibar.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>