Na Madina Issa
WENYEVITI wa CCM mikoa sita kichama, wameziomba serikali zote mbili kuendeleza juhudi kuhakikisha amani na utulivu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Haji Juma Haji, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi ya mkoa Amani wilaya ya mjini Unguja.
Alisema serikali zisitoe mwanya kwa mtu yeyote au kikundi fulani chenye lengo la kuvuruga amani na utulivu kwa maslahi binafsi.
Alisema Zanzibar inaongozwa na misingi ya demokrasia na utawala wa sheria hivyo avitaka vyama vya upinzani kuacha vitisho na uchochezi wenye lengo la kuvuruga amani na utulivu uliopo.
Akizungumzia mchakato wa katiba mpya,alisema katiba mpya itapatikana kwa nguvu ya hoja zitakazojengwa ndani ya bunge.
Aliwataka wapinzani kuandaa hoja madhubuti zitakazowaelimisha wananchi juu ya mfumo wa serikali itakayokuwa na maslahi kwa vizazi vijavyo na taifa kwa ujumla.
Pia aliwataka wanachama wenzake hasa vijana kuwa macho na njama za baadhi ya vyama vya upinzani ambapo kwao Mapinduzi ni janga.