Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Kituo cha Redio cha Al-Noor Chaunguwa kwa Moto maeneo ya Mtoni Daraja Bovu.

$
0
0
Jengo la Ofisi za Kituo cha Redio cha Al Noor , sehemu hii inayotumika na kituo hicho ikiwa imeteketea kwa moto uliotokea usiku wa juzi na kusababisha hasara na mmoja wa Mfanyakazi wake aliyekuwa zamu kujeruhiwa na moto huo baada ya kuruka kutoka gorofa ya kwanza na kupata majaraha makubwa. na kulazwa hospitali ya Mnazi mmoja 
    Moja ya mashine za kituo hicho ikiwa imeharibika kwa moto huo.
Sehemu ya koridoo ya Ofisi hiyo ikiwa imeteketea kwa moto kama inavyoonekena pichani.
Waya wa Umeme ukiwa umeungua na moto huo, unaosadikiwa na kusababishwa na hitilafu ya umeme iliokikumba kituo hicho na kusababisha hasara kubwa. 
                   Studio ya Redio Al Noor ikiwa imeteketea kwa moto huo.

Studio ya kutangazia ya Kituo hicho ikiwa imeharibika vibaya sana kwa moto uliotokea usiku wa manani katika kituo hicho na kusababisha mfanyakazi wa kituo hicho kuvunjika mguu na majaraha mengine akiwa amelazwa hospital kuu ya mnazi mmoja akipata matibabu.

Kituo cha kurushia matangazo cha redio Al-Noor kilichopo Mtoni Kidatu wilaya ya magharibi Unguja kimeungua moto usiku wa kuamkia jana na kusababisha hasara inayokisiwa kufikia shilingi milioni 80.

Mkurugenzi wa redio hiyo, Mohammed Suleiman, alisema moto huo inawezekana ukawa umesababishwa na hitilafu za umeme.

Alisema moto huo umeteketeza maeneo yote ya studio zao zote tatu za redio hiyo na vitu mbalimbali vilivyomo ndani ya studio hizo.

Akivitaja vitu hivyo Mkurugenzi huyo alifahamisha kuwa ni studio namba moja, studio namba mbili na studio namba tatu ambayo ni studio kubwa kwa ajili ya kurushia matangazo na vitu vingine vilivyoungua ni mashine za kurushia matangazo, kompyuta za kurikodi, mafeni, mazulia na vitu vingine viliopo ndani ya studio hizo.

“Moto umetokea usiku wa saa 8 tunasema inawezekana ikawa umesababishwa na shoti ya umeme japo kuwa hatujathibitishiwa na watu wa umeme lakini mwanzo ulikuwa umezimwa na ulipowashwa ndipo ilipotokea shoti hiyo na kuunguza vitu mbalimbali ambavyo vilikuwa vikitumika kwa kuendeleza kazi zitu za redio”, alisema.

Alifahamisha kuwa studio namba tatu ni studio kubwa ya kurushia matangazo hivyo studio hiyo imeungua vitu vyote na kusababisha hasara inayokisiwa ni zaidi ya milioni 52.

Mkurugenzi huyo alifahamisha kuwa kutokana na hali hiyo na hasara waliyoipata kituo hicho hivi sasa kimesimamisha matangazo yake kwa muda hadi pale watapoweza kukamilisha matengenezo na manunuzi ya vifaa vilivyoungua. 
Alisema kituo hicho si mara ya mwanzo kuungua kwani siku za nyuma kimeshawahi kuungua lakini hasara haikuwa kubwa.
Mbali ya hasara hiyo, alisema mfanyakazi wao Abubakar Fakih, amejeruhiwa kwa kuvunjika mguu na mkono baada ya kuruka ili kujinusuru.
“Mfanyakazi wetu toka aumie tupo nae pamoja na yupo hospitali kuu ya Mnazimmoja na amefanyiwa upasuaji,” alisema.
Aidha alisema vitabu vitatu vitakatifu (Quran) ambavyo vilikuwa ndani ya studio zilizoungua, havikuguswa na moto huo.
Aidha alisema kituo hicho hakitarusha matangazo yake kwa sasa hadi matengenezo yatakapofanywa.

Alitumia nafasi hiyo kuwataka waumini, wafadhili na watu wenye uwezo kuisaidia redio hiyo. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>