Na Asya Hassan
JESHI la Polisi Zanzibar linawashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kuwa majambazi ambao wanadaiwa kuvamia hoteli ya Milele Villa iliyopo Fukuchani wilaya ya kaskazini ‘A’ mkoa wa kaskazini Unguja.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Yusuf Ilembo, tukio hilo limetokea Machi 26 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku huko Fukuchani.
Alisema majambazi hao hawakujulikana lakini wanakisiwa walikuwa zaidi ya wanne ambao wakiwa na bunduki aina ya SMG, walivamia hoteli hiyo na kumnyang’anya mmiliki wa hoteli hiyo fedha za kitanzania shilingi 250,000 pamoja na dola za Marekani 3,500.
Alivitaja vitu vingine alivonyang’anywa ni laptop moja a ina ya CCA yenye thamani ya Euro 600, nyengine ni aina ya Samsung yenye thamani ya Euro 1000, camera moja yenye thamani ya Euro350, saa ya mkononi yenye thamani ya Euro 100, neckless forth ladly yenye thamani Euro 50, simu mbili aina ya Samsung zenye thamani ya Euro 150 na simu ya nokia ikiwa yenye thamani ya dola za Marekani 450.
Alisema katika tukio hilo hakuna mtu aliyejeruhiwa lakini walifanikiwa kuokota ganda moja la risasi ya SMG.
Alisema kukamatwa kwa majambazi hayo kunatokana na taarifa za uhakika na kushirikiano na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wema.
Alisema jeshi limefanikiwa kuwakamata majambazi hao na katika kuwapekua, walikutikana na bunduki mbili.
Alisema bunduki hizo ni SMG namba AB 3903 na risasi 31 na nyengine ni bastola aina ya browning namba SW 6092 na risasi zake tisa.
Alisema bunduki hizo ndizo zilizotumika Machi 2 mwaka huu katika tukio la mauaji la askari polisi lililotokea hoteli ya Pongwe Bay Resort.