Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Shirika lafutwa kwa kueneza ushoga

$
0
0
Na Mwandishi wetu

SERIKALI ya Tanzaniaimefutilia mbali usajili wa shirika moja lisilokuwa la kiserikali kwa sababu ya kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja katika jamii.

Shirika hilo la Sisi Kwa Sisi lilisajiliwa baada ya kudai kuwa malengo yake yalikuwa ni kusaidia jamii.

Serikali ilisema imechukua hatua ya kufutilia mbali usajili wa shirika hilo kwa kukiuka sheria za nchi na kwenda kinyume na malengo ya usajili wake.


Mkurugenzi wa usajili wa mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Tanzania, Maseli Katemba, alisema shirika hilolimekiuka malengo yake ya awali ya kuwapa elimu na misaada ya kifedha wananchi lakini mambo yakawa tofauti.

"Baada ya kufuatilia tumegundua kuwa sasa wanatilia mkazo kuwasaidia watu wa jinsia moja," alisema Katemba.

Alisema serikali itaendelea na kuyasaka makundi mengine kama hayo ambayo yanaendesha maswala yaliyo kinyume na sheria za Tanzania.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>