Quantcast
Channel: ZanziNews
Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Mvua yaleta maafa Arusha

$
0
0
Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
MVUA kubwa iliyonyesha wilayani Karatu imesababisha mafuriko makubwa na  mto Mlera kujaa maji ambapo gari zaidi ya 100 zilishindwa kuvuka, huku dereva wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, (NCAA), Juma Moshi, akinusurika kufa baada ya kusombwa na mafuriko.

Hata hivyo, Mkuu wa Idara ya Huduma ya Uhandisi wa NCAA, Isra Missana, pamoja na wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo wakishirikiana na wakazi jirani wa eneo hilo, walifanikiwa kumwokoa dereva huyo majira ya saa 12:30 asubuhi.

Katika hatua nyingine, mamia ya wasafiri waliokuwa wakitoka maeneo ya Karatu na watalii waliokuwa wakitoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwenda mjini Arusha, Dar es Salaam na maeneo mengine nchini  walikwama kwa saa 6 hadi mchana maji yalipopungua na kuvuka.

Mto Kirurumo pia ulifurika maji hadi kupita juu ya barabara huku ukiporomosha mawe makubwa kutoka milima ya Mbulumbulu na kusababisha hofu kwa wakaazi wa eneo hilo.


Mto huo upo mpakani mwa wilaya ya Monduli na Karatu.
Miongoni mwa abiria walioshindwa kusafiri ni wale waliokuwa wasafiri kwa basi la Dar Express ambalo mapema asubuhi lilionekana likirudi tena mjini Karatu baada ya kushindwa kuvuka katika  mto huo.

Abiria wengine waliotakiwa kusafiri kwa basi la Sai Baba halikuweza kuanza safari yake ya kwenda Dar es Salaam.
Mamia ya gari zilizokuwa zikiwasafirisha watalii kutoka hifadhi za taifa zilikuwa miongoni mwa gari zilizokwama katika eneo hilo.

Mto Kirurumo unamwaga maji yake katika Ziwa Manyara lililopo katika Hifadhi ya Taifa ya Manyara.

Mafuriko hayo yalitokana na mvua kubwa iliyonyesha maeneo ya Milima ya Mbulumbulu juzi usiku hadi kuamkia asubuhi.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Felix Ntibenda, akizungumza katika eneo la tukio hillo alisema tatizo la mafuriko katika mto huo limekuwa likijirudia mara kwa mara.


Alisema serikali inafanya utafiti wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la mafuriko yanayoporomosha mawe na kuharibu barabara hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 35043

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>