Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu Chungu na Vibuyu, vilivyotumika kuchanganya Udongo wa Tanganyika na Zanzibar, mwaka 1964, kutoka kwa Mawazo Ramadhan wa Makumbusho ya Taifa, wakati alipotembelea kwenye Banda la Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, alipotembelea maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Ofisa wa Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Mashuki, baadhi ya Magazeti yaliyochapishwa mwaka 1964, wakati alipotembelea kwenye Banda la Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, alipotembelea maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kuhusu shughuli za Bunge kutoka kwa Ofisa Habari wa Bunge, Prosper Minja, wakati alipotembelea kwenye Banda hilo, kwenye maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, apata maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Magishi Mgasa, alipokuwa akitembelea kwenye Mabanda ya maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na OMR