JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706 FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 16 Aprili, 2014
Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa. Taarifa Na. | 201404-02 |
Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki | Saa 10:00 Alasiri |
Daraja la Taarifa: | Tahadhari |
Kuanzia: Tarehe | 17 Aprili, 2014 |
Mpaka: Tarehe | 18 Aprili, 2014 |
Aina ya Tukio Linalotarajiwa | Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24, ukanda wa pwani. |
Kiwango cha uhakika: | Wastani (70%) |
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika | Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga, Pwani na Dar es Salaam. |
Maelezo: | Kuimarika kwa ukanda wa mvua "Inter-tropical convergence zone (ITCZ)" ambao umeambatana na ongezeko la unyevunyevu na kuwepo kwa ‘Easterly Wave’. |
Angalizo: | Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki. |
Maelezo ya Ziada | Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi. |