Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe wakiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasa la awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na viongozi hao waliokuwa wakielekea kuhani msiba wa kada wa CCM Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasala awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na na baadaye kutelemka na Rais aliyekuwa akielekea kuhani msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika Kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada. Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuhani na kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo April 17, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam leo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, wakiangalia cheti cha heshima alichopewa na Gavana wa Maryland wakati wa kupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membekupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kupokea toka kwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membekupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.( Picha na Ikulu )