Na Mwandishi Wetu.
Umoja wa taasisi mbalimbali za kiraia Tanzania (AZAKI) umesema watanzania hawajapendezwa na vitimbi na maneno ya kashafa ya wajumbe wa bunge la katiba huku fedha za umma zikipotea pasipo na jambo la maana.
Katika taarifa yao ya pamoja juu ya mjadala wa katiba unaoendelea huko Dodoma kuwa wajumbe hao wamepoteza utaifa na badala yake wamejikita kwenye ubaguzi,ubabe,vijembe na vitisho vya kutoheshimiana kinyume na matakwa ya mkutano huo.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini dar es salaam mwenyekiti wa umoja huo Irenei Kiria amesema taasisi hizo zimehuzunishwa na tabia ya kudhihaki na kudhara rasimu ya pili ya katiba pamoja na tume ya katiba na hasa Mwenyekiti wake Jaji Warioba, aliyekusanya maoni ya wananchi kuhusu uundwaji wa katiba mpya.
Amefafanua kuwa inasikitisha mwenendo wa mijadala ya bunge hilo inaelekea kutetea maslahi ya watakwa na vyama siasa na makundi binafsi badala ya maslahi ya ya taifa na ustawi wa wananchi inayosababisha masuala madogo kuchukuwa muda mrefu kitendo kinachotakiwa kutofumbiwa macho.
Umoja wa asasi hizo zipatazo 500 za Tanzania umewasihi wajumbe wa bunge maalum la katiba pamoja na uongozi wa bunge hilo kurekebisha kasoro zilizoorodheshwa na na taasisi hizo ,ili kupata katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi wenyewe na si kuhatarisha amani ya nchi